Shughuli zetu:

Taasisi ya Sayansi Jamii (TASAJA) pia inajulikana kama Chama cha Wanasosholojia Tanzania, Ilianzishwa mwezi Novemba, 2013 chini ya Sheria ya Vyama (2002) na kupewa usajili SA 19074 na Ni mwanachama wa Vyama vya Wanasosholojia kimataifa kimesajiliwa mwezi Machi., 2014.
Uanachama wa chama ni wazi kwa wahitimu wote wa Sociology; kutoka taasisi ambayo inatoa digrii ya sosholojia kwa ajili ya kujifunzia; watu binafsi au Makundi ambao wapo tayarikujiunga na mkondo wake,


1 Kuendeleza malengo ya Sayansi Jamii katika  jamii yetu kwa kutoa elimu. Kufanya utafiti, kuhusiana na maisha ya watu, mienendo yao na mazingira kwa ujumla wake.


.2. Kujenga maelewano na ushirikiano baina ya makundi mbalimbali kwenye jamii.


.3. Kufanya utafiti wa maswala yote yanayiihusu jamii kama tabia na mienendo ya mwanadamu, mazingira na maisha ya kila siku kuanzia kwenye kaya, mtaani,na dunia nzima


.4. Kupitia kazi za kitafiti kwa lengo la kuziandaa kwa ajili ya kuzichapisha na kuzitawanya katika jamii na kusambaza matokeo ya utafiti huo kwenye jamii.

5. Kutoa huduma za kiushauri katika mambo yote ya kijamii yanayohusiana na Sayansi ya jamii kama ilivyo ainishwa kwenye tamko letu