Hali ya Taasisi:
 

 

KATIBA YA TAASISI SAYANSI JAMII
(TASAJA)

TAASISI YA KUENDELEZA MALENGO YA SAYANSI JAMII

IMETAYARISHWA NA WANACHAMA WA TASAJA
APRILI, 2013

 

YALIYOMO
TAMKO.............................................................................                3
1.0 Jina na makao makuu ya taasisi..................................               4
2.0 Malengo ya taasisi.......................................................               4
3.0 Muundo wa taasisi......................................................                4
4.0 Uanachama................................................................                5
5.0 Uongozi.......................................................................     …       6
6.0 Baraza la wadhamini....................................................               7
7.0 Bodi ya wakurugenzi.....................................................              7
8.0 Vikao vya taasisi...............................................................          7
9.0 viongozi wa taasisi.........................................................              9
10.0 Raslimali za taasisi........................................................           10
11.0 Marekebisho ya katiba................................................             11
12.0 Kuvunjwa kwa taasisi....................................................            11
13.0 Mgawanyo wa mali za, madeni ya,  na fedha za taasisi…        11

TAMKO:
Kwa kuwa tunatambua kwamba sayansi ya jamii:

 • ni elimu inayohusu ya jamii
 • ni elimu inayohusu maisha ya watu, makundi ya watu, na jamii yote.
 • ni elimu inayohusu tabia na mienendo ya mwanadamu, katika Nyanja zote katika mahusiano, mazingira na maisha ya kila siku, kuanzia kwenye kaya, mtaani, dunia nzima.
 • ni elimu inayohusu mambo yote yanayoigusa jamii huku yakimuhusu mwanadamu katika maisha yake yote, urefu wa uhai wake, na hata baada ya uhai wake.
 • ni elimu inayogusa na kuunganisha  elimu na maarifa yote yanayomhusu mwanadamu

Kwa hiyo sisi wanachama wa taasisi ya sayansi ya jamii tunaamua kuanzisha taasisi hii ili kuweza kutafasiri kwa vitendo malengo ya sayansi ya jamii katika jamii yetu ili kujenga jamii inayojitambua, inayotambua tunu zake, iliiweze kuzitumia tunu hizo kuondoa umaskini, na kujenga jamii yenye maelewano, maendeleo endelevu, na ustawi.

1.0 Jina na makao makuu ya taasisi

1.1 Jina la Taasisi: TAASISI  YA SAYANSI JAMII (TASAJA)
1.2 Makao makuu ya taasisi: MAKAO MAKUU YA TAASISI YATAKUWA MWANZA
1.3 ANUANI YA TAASISI ITAKUWA
TASAJA
Bwiru Mchangani
S.L P.2825
MWANZA.

2.0 Malengo ya Taasisi

2.1 Kuendeleza malengo ya Sayansi Jamii katika  jamii yetu kwa kutoa elimu. Kufanya utafiti, kuhusiana na maisha ya watu, mienendo yao na mazingira kwa ujumla wake.
2.2. Kujenga maelewano na ushirikiano baina ya makundi mbalimbali kwenye jamii.
2.3. Kufanya utafiti wa maswala yote yanayiihusu jamii kama tabia na mienendo ya mwanadamu, mazingira na maisha ya kila siku kuanzia kwenye kaya, mtaani,na dunia nzima
2.4. Kupitia kazi za kitafiti kwa lengo la kuziandaa kwa ajili ya kuzichapisha na kuzitawanya katika jamii na kusambaza matokeo ya utafiti huo kwenye jamii.

2.5. Kutoa huduma za kiushauri katika mambo yote ya kijamii yanayohusiana na Sayansi ya jamii kama ilivyo ainishwa kwenye tamko letu (ukurasa 3).

3.0 Muundo wa Taasisi

Taasisi itakuwa na sehemu kuu zifuatazo

 • Wanachama
 • Uongozi:
 • Bodi ya wakurugenzi
 • Bodi ya wadhamini

4.0 Uanachama

4.1 Sifa za uanachama

(a) Wahitimu wa sayansi ya jamii
(b) Watu wote wanaokubaliana na malengo ya taasisi
(c) Taasisi zinazotoa mafunzo ya sayansi ya jamii

4.2 Aina za uanachama

 • Mtu mmoja mmoja
 • Kikundi watu au
 • Taasisi zinazotoa mafunzo ya sayansi ya jamii

4.3 Jinsi ya kuwa mwanachama

 • Mwanachama atajaza fomu ya maombi yakuwa mwanachama nakuambatanisha ada ya maombi ya uanachama.
 • Muombaji akikubaliwa kujiunga baada yakutimiza masharti, atalipa kiingilio cha uanachama ambacho hakitarejeshwa.

4.4 Wajibu wa mwanachama

 • Kulipa ada na michango
 • Kushiriki katika shughuli mbalimbali za taasisi katika azima yakutimiza malengo yake.

 

4.5 Haki za mwanachama

 • Kushiriki katika shughuli zote za taasisi.
 • Kushiriki katika vikao vyote vinavyomhusu
 • Kutobaguliwa kwa namna yoyote ile
 • Haki yakutoa maoni na kusikilizwa
 • Haki ya kuchagua/kuchaguliwa mjumbe/kiongozi

4.6 Ukomo wa uanachama

 • uanachama utakoma endapo:

 

 • Mwanachama atajitoa mwenyewe
 • Atashindwa kutimiza masharti ya uanachama
 • Kwa utovu wa nidhamu
 • Atathibitika kuwa na Maradhi ya akili
 •  Ataenda kinyume cha katiba ya taasisi

 

 • Mwanachama atafariki
 • Atatoa, kushawishi au kupokea rushwa ya aina yeyote ile.

 

5.0  Uongozi

        Umoja utakuwa na viongozi wafuatao:-

 • Mwenyekiti
 • Mwenyekiti Msaidizi
 • Katibu
 • Katibu Msadizi
 • Mweka Hazina

5.1   Sifa za Kiongozi:

 • Awe mwaminifu na mwadilifu.
 • Awe na uwezo wa kusimamia na kutekeleza maazimio ya vikao vya taasisi.
 • Awe na uwezo wa kuilinda, kuitetea na kutekeleza katiba.
 • Awe na uwezo wa kuonyesha hekima na kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa na ustawi wa taasisi.
 • Awe na uwezo wa kuunganisha na kuhamasisha wananachama kutimiza malengo ya taasisi.
 • Awe ni mfano mzuri wa kuigwa katika kuzingatia katiba.
 • Mweka Hazina awe na elimu au ufahamu wa uhasibu.

5.2   Uchaguzi wa Viongozi:

 • Uchaguzi wa viongozi utafanyika kwa kupiga kura ya siri na mgombea atakayepata kura nyingi ndiye mshindi.
 • Endapo atajitokeza mgombea mmoja atapigiwa kura ya ndiyo au hapana.
 • Mwanachama atastahili kugombea endapo atakuwa ametimiza masharti ya katiba ya taasisi.

5.3   Muda wa Uongozi:

 • Muda wa uongozi utakuwa miaka mitatu isipokuwa kiongozi yeyote anaweza kusimamishwa au kuachishwa uongozi endapo atakiuka maadili ya uongozi au kupungukiwa sifa za uanachama kwa mujibu wa katiba hii.
 • Kiongozi aliyemaliza muda wake anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine kimoja ili mradi asiwe madarakani kwa zaidi ya vipindi viwili mfululizo.

 

6.0 Baraza la wadhamini
Watu wasio wanachama wa taasisi ambao watateuliwa na mkutano wa wanachama wote ili kufanya kazi kama baraza la wadhamini.

  • Kazi za baraza la wadhamini

Wadhamini watakuwa na wajibu wa:-

 • kutoa ushauri,
 • kusuluhisha migogoro
 • kuijengea taasisi uwezo
 • kusimamia uvunjaji wa taasisi.

6.2 Muda wa baraza la wadhamini

Baraza la wadhamini litafanya kazi kwa muda wa miaka mitatu (3) sawa na kipindi cha uongozi.

7.0 Bodi ya wakurugenzi

Bodi ya wakurugunzi itaundwa na:-
a). watu watakao chaguliwa na mkutano mkuu wa wanachama wote, kutoka nje ya taasisi
b). wanachama wa taasisi watakao ingia kwa mujibu wa nyadhifa zao.
7.1 Kazi za bodi ya wakurugenzi
a). Kubuni dhima, sera na malengo ya taasisi.
b).Kutafuta rasilimali za kuhakikisha dhima, malengo na sera za taasisi zinafikiwa.
c).Kuhakikisha taasisi inakuwa raia mwema.
d).Kuhakikisha taasisi inafuata na kutimiza masharti yote na wajibu wote kama ilivyoelekezwa na sheria za nchi.
e).Kuhakikisha kuwa malengo ya taaluma ya sayansi ya jamii yanafuatwa.

8.0  Vikao vya taasisi

Taasisi itakuwa na vikao vifuatavyo:

 • Mkutano mkuu,
 • Mkutano wa sekretarieti
 • Mkutano wa bodi ya wakurugenzi.
 • Mkutano wa robo mwaka

8.1 Mkutano mkuu

Mkutano mkuu
a).ndio kikao kikuu kabisa cha taasisi.
b).Utajumuisha wanachama wote wa taasisi

8.1.1 Kazi za mkutano mkuu:

a).Kuchagua viongozi wa taasisi
b).Kuchagua bodi yawakurugenzi ya taasisi

 

 

c).Kuchagua bodi ya wadhamini ya taasisi
d).Kuteua wanachama watakao unda vikao vya sekretarieti
e).Kupitisha ripoti ya shughuli, mapato, na matumizi ya taasisi kwa mwaka.
f).Kupitisha dhima, dira na sera za taasisi
g). Kuteua wanachama wawili watakaotia saini kwenye malipo ya taasisi
h) Kupanga muda na mahali utakapofanyika mkutano utakaofuata.
i). Kupitisha katiba
j). Kupitisha mabadiriko ya katiba

8.1.2 Vikao vya mkutano mkuu

Kutakuwa na mkutano mkuu wa mwaka. 

Kutakuwa na mkutano wa dharura

8.1.3 Utaratibu wa mkutano mkuu.

Mwenyekiti wa mkutano mkuu  atakuwa Mwenyekiti wa taasisi. Kama hayupo makamu mwenyekiti atakuwa mwenyekiti wa muda na endapo hatakuwepo mwanachama yeyote atachaguliwa na wanachama wenzake kuwa mwneyekiti wa muda.

8.1.4 Utaratibu wa maamuzi

Maamuzi yote yatakuwa kwa njia ya kura za siri, ili yafikiwe lazima yazidi nusu ya kura zote zilizopigwa.

8.2 Vikao vya sekretarieti

Vikao vya sekretarieti vitafanyika mara moja kila mwezi au kwa kadri wanavyo ona inafaa.

8.2.1 Vikao vya dharura

Vikao vyote vya dharura vitafanyika kila inapobidi

8.3 vikao vya bodi ya wakurugenzi

Vitakaa kabla ya mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wote.
8.4 vikao vya robo mwaka
Vikao hivi vinaundwa na wanachama wote
Vikao hivi ni kwa mjibu wa sheria na kanuni za usajili wa taasisi za jamii. Pamoja na  kuzingatia sheria na kanuni hizo , vikao hivi vitakuwa na wajibu:-

  • Kuandaa taarifa ya utendaji wa taasisi ya robo mwaka
  • Kuandaa taarifa ya fedha ya robo mwaka
  • Kuandaa taarifa ya hali na uhai wa taasisi ya robo mwaka

 

 

 

 

 

8.5 Akidi ya vikao

Akidi ya vikao vyote vya taasisi itakuwa theluthi mbili ya wajumbe.

9.0 Viongozi wa taasisi

Viongozi wote watachaguliwa kila baadaya miaka mitatu na watachaguliwa kwenye mkutano mkuu wa taasisi.

9.1 Mwenyekiti.

Mwenyekiti:
a). Atakuwa ndiye msemaji mkuu wa taasisi.
b) Atachaguliwa kwa zaidi ya nusu ya kura zote zitakazo pigwa.
c).Atakua uongozini kwa muda wa miaka mitatu, na anawezi kuchaguliwa kwa mara nyingine kuongoza taasisi katika ngazi hiyo.
d).Atakuwa mwenyekiti wa vikao vyote vya sekretarieti na mkutano mkuu.
e). Ataondolewa kwenye wadhifa wake kwa kura ya kutokuwa na imani nae na ataondololewa kwa theluthi mbili ya akidi ya kikao cha wanachama wote.
f).Atahusika katika kusaini hati za malipo yote ya taasisi.
9.2 Makamu mwenyekiti.
Makamu Mwenyekiti
a).Atakaimu nafasi na kazi za mwenyetiki endapo Mwenyekiti atakuwa hayupo.
b).Atachaguliwa kwa zaidi ya nusu ya kura zote zitakazopigwa.
c).Atakua uongozini kwa muda wa miaka mitatu, akimaliza mda wake, anaweza kuchaguliwa tena endapo wanachama wataamua.
d). Ataondolewa kwenye wadhifa wake kwa kura ya kutokuwa na imani nae na ataondololewa kwa theluthi mbili ya akidi ya kikao cha wanachama wote.

9.3 Katibu

Katibu mkuu
a).Atachaguliwa kwenye mkutano mkuu wa wanachama wote.
b).Ndiye mtendaji mkuu wa shughuli zote za taasisi. Atakuwa na wajibu wa kutunza nyaraka za vikao na mali za taasisi.
c).Atahusika na kusaini hundi za taasisi kutoka kundi A.
d) Atachaguliwa kwa zaidi ya nusu ya kura zote za mkutano mkuu.
e).Ataondolewa kwenye wadhifa wake kwa kura ya kutokuwa na imani nae, na ataondolewa kwa theluthi mbili ya akidi ya kikao cha wanachama wote. Atakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu tu.
9.4 Naibu katibu.
a).Atakaimu nyadhifa na shughuli zote za katibu endapo hatakuwepo.
b) Atachaguliwa kwa zaidi ya nusu ya kura zote za mkutano mkuu.
c). Ataondolewa kwenye wadhifa wake kwa kura ya kutokuwa na imani nae, na ataondolewa kwa theluthi mbili ya akidi ya kikao cha wanachama wote.
d). Atakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu tu.     
9.5 Mhazini
Mhazini
a).Atachaguliwa na mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama wote.
b).Atakuwa mtunza nyaraka zote zinazohusu fedha.
c).Atawajibika kwa Mwenyekiti.
d).Ataondolewa kwenye wadhifa wake kwa kura ya kutokuwa na imani nae na ataondolewa kwa theluthi mbili ya akidi ya kikao cha wanachama wote.
e).Atakaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu tu.
f). atakuwa mmoja wa waweka saini katika malipo ya taasisi katika kundi A.

10.0 Rasilimali fedha

10.1 Vyanzo vya fedha

Vyanzo vya fedha vya taasisi vitakuwa ni:
a). Tozo mbalimbali kama faini kwa makosa mbalimbali na huduma zitakazotolewa na taasisi.
b).Ada,
c) Michango ya hiari
d)  Mikopo
10.2Utunzaji na malipo
Fedha za taasisi zitatunzwa benki, kwenye akaunti ya taasisi. Malipo yote yatafanyika kutoka au kupitia benki.

10.3Ukaguzi wa mahesabu

 Hesabu za taasisi zitakaguliwa na mkaguzi mahesabu wa nje atakae teuliwa na mkutano mkuu wa wanachama wote kila mwaka.

10.4Taarifa ya mapato na matumizi

Taarifa ya mapato na matumizi itaandaliwa na kupelekwa kwenye mkutano wa wanachama wote.

10.5 Watia saini

Watia saini wa malipo ya taasisi watakuwa
a).Katibu,
b).Mweka hazina
c).Wanachama wawili watakao teuliwa na Mkutano Mkuu.
10.6 utaratibu wa watia saini
a).Katibu na mweka hazina watakuwa kundi A
b). Wanachama wawili watakuwa kundi B
c). malipo halali sharti yasainiwe na mtia saini mmoja kutoka kundi A na Mwaingine kutoka kundi B
d). Hati ya malipo sharti isainiwe na Mwenyekiti wa taasisi au mtu anayekaimu nafasi yake.

11.0 Marekebisho ya katiba

Hoja za mabadiliko ya katiba zitaletwa mezani na sekretarieti na wanachama wengine. Katiba itabadilishwa kwa uamuzi wa mkutano mkuu utakao fikiwa na theluthi mbili (2/3) ya wanachama wote.

12.0 Kuvunjwa kwa taasisi

Taasisi itavunjika baada yakufikiwa maamuzi ya kura za wanachama wasiopungua robo tatu (3/4) chini ya usimamizi wa baraza la wadhamini.
13.0 Mgawanyo wa mali za, madeni ya, na fedha za  taasisi
a). Kama taasisi inadaiwa mali zake zitauzwa ili kulipa madeni.
b). Kama taasisi haitakuwa inadaiwa mali zitahamishiwa kwa taasisi zingine za kijamii zenye malengo sawa na/au mahusiano na taasisi.
c). akiba ya fedha itangawanywa sawa kwa wanachama.

14.0 Utatuzi wa migogoro

Migogoro yote itatatuliwa kwa njia ya vikao vya bodi ya wakurugenzi na hatimaye kwenye mkutano mkuu wa wanachama wote.